Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Godfrey Ngupula ameshangazwa na ujasiri walionao wananchi wanaolima mashamba makubwa ya bangi kwa kujiamini kama hakuna serikali.
“Sijawahi kuona watu wanalima bangi kwa kujiamini kiasi hiki tena kwa wingi kama hakuna Serikali, tutahakikisha bangi yote inateketezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani,” alisema Ngupula
Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nzega, Costantine Mbogambi alisema jeshi hilo litapiga kambi msituni kuhakikisha mashamba yote yanateketezwa.
