Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA kanda ya Dar es Salama imesema kumekuwepo na ongezeko kubwa la uanzishwaji wa vyuo vya ufundi stadi kiholela ambavyo vinatoa huduma chini ya viwango na hivyo imetangaza operesheni maalum ya kuvisaka vyuo vyote ambavyo vinajiendesha kinyume na sheria na watavichukulia hatua za kisheria ikiwemo kuvifungia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga amesema kutokana na kuwepo kwa vyuo holela matokeo yake vimekuwa vinazalisha wataalamu ambao hawaendani na hali halisi mahitaji ya soko kwa sasa.
Naye mkurugenzi wa kanda hiyo Bw. Habibu Buko amesema wanachofanya sasa hivi ni kujitathimini na kuweza kuzalisha wataalamu ambao wanaweza kuendana na uchumi wa viwanda ambao ndio agenda ya sasa ya serikalini na hivyo wanajukumu kubwa mbele yao.
Wakati VETA wakiyasema hayo umoja wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam amesema wanachoataka kutoka VETA ni kuona mamlaka hiyo inakuwa na mfumo wake unaojitegemea ili kutoa huduma bora tofauti na ilivyo sasa kuwa baadhi ya majukumu ya VETA yanaingiliwa ama yanaingia katika nyanya zingine.