Barnaba
Mkali wa bongo fleva Barnaba Classic ambaye anatamba kwa kibao chake matata kinachopewa jina la 'Lonely' usiku wa kuamkia leo Jumatatu amelizwa vitu vilivyokuwa ndani ya gari lake na watu wasiojulikana.
"Naomba sana sana waungwana kama kuna mtu yotote atabaini au kujua vilipo au hata kupelekewa basi naomba wasamalia wema mnirudishie au kuniletea napatikana kwa 'No 0743505010' Mungu awabariki naamini aliyenavyo hajaiba bali amepitiwa katika njia ya kutafuta riziki nami kwa jina la Mungu nitamsamehe na nimesamehe ila kama ana rohoo nzuri na ameguswa basi naomba waungwana mnipigie hata kama umeokota". Ameandika Barnaba
