Ucheleweshwaji wa Pembejeo za ruzuku kwa wakulima mkoani Katavi umeibua mjadala mkali baina ya wadau wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa katavi kutokana na hali hiyo kudhoofisha wakulima na kupata matokeo hasi kwa baadhi ya maeneo ambapo matarajio ya mavuno kwa mwaka 2017/2018 yameshuka kwa zaidi ya asilimia sita huku mkoa huo ukitegemewa na mikoa mikoa mingine katika uzalishaji wa mazao chakula.
Wadau hao wameoneshwa kusikitishwa na ucheleweshwaji wa pembejeo za ruzuku katika sekta hiyo muhimu inayotegemewa na zaidi ya asilimia 80% ya wakazi wa mkoa huo huku mikoa mingine hasa ya kanda ya ziwa ikitegemea kununua mazao ya chakula kutoka mkoani katavi.
Aidha hali hiyo imeelezwa kuwaumiza wakulima wengi wa kipato cha chini kutokana na kukosa fedha za ununuzi wa mbegu ama mbolea na hivyo kujikuta wanalazimika kuendeleza kilimo kisicho na tija.
Katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Katavi Bwana. Awariywa Nnko amesema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 japo mkoa uliweka utaratibu mzuri wa ugawaji wa pembejeo hizo za ruzuku bado kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwemo ucheleweshwaji wa mbegu na mbolea za kupandia.