Wawekezaji wanaokiuka sheria za kazi nchini wapewa onyo

Serikali imetoa onyo kwa wawekezaji wanaokiuka sheria za ajira na zile za utunzaji wa mazingira ambapo imeahidi kuanza kuwachukulia hatua kali na zakisheria ikiwa ni pamoja na kufunga  viwanda  vyote vitakavyobainika kukiuka sheria hizo.

Wakati serikali ya Tanzania ikipambana kutafuta wawekezaji wenye tija kwa taifa kuja kuwekeza nchini  na kuongeza ajira kwa vijana  wa kitanzania, kiwanda cha king dao kinachomilikiwa na raia wa kichina kinazalisha maji huku kikikiuka sheria za kazi kwa kuwalipa wafanyakazi wake shilingi 6000 kwa kutwa.

Katika kiwanda hiki maafisa wa serikali wamebaini mapungu lukuki  ya kiwemo ya wafanyakazi  kutokuwa na  mikataba, ukiukwaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004, ambapo licha ya kukifunga kiwanda hicho pia maafisa waserikali wakatangaza kukipiga faini ya shilingi milioni 20.

Kwa upandewake naibu waziri wa kazi vijana na ajira ambaye ndiye aliyeongoza oparesheni hiyo ya kushitukiza katika kiwanda hicho cha king dao, amesema hatasita kufunga viwanda vyote vitakavyobainika kukiuka sheria za kazi hasa kwa kushindwakuwapatia mikataba wakazi wake.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia