Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa anatarajiwa kufungua mkutano wa tisa wa wadau wa mfuko wa pensheni wa LAPF unaotarajiwa kuanza machi 9 jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini humo, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa mfuko wa LAPF, James Mlowe amesema mkutano huo utashirikisha wadau wote wa mfuko huo ambapo wanachama zaidi ya elfu moja watashiriki mkutano huo na, katika mkutano huo Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo uendeshaji wa mfuko, pamoja na mahesabu yaliyokaguliwa na mkaguzi wa hesabu za serikali kwa kipindi cha mwaka husika.
Mlowe amesema kuwa, mbali na kujadili utendaji kazi wa mfuko huo na uwekezaji wake kutakuwepo na wataalamu watakaotoa Mada ya ugonjwa wa figo kwa kuwa siku hiyo imeangukia siku ya figo duniani ambapo kupitia wataalamu hao wananchi watapimwa bure.