WHO: Tatizo la kifua kikuu bado ni changamoto duniani

Ugonjwa wa kifua kikuu au TB bado ni changamoto kubwa duniani na kwa kulitambua hilo shirika la afya ulimwenguni limetoa muongozo mpya wa kimaadili likiadhimisha siku ya kifua kikuu ambayo hua Machi 24 kila mwaka.

Baadhi ya mambo yaliyojumuishwa katika muongozo huo wa WHO ni masuala ya kutengwa kwa wagonjwa wa kuambukiza, haki ya wagonjwa wa kifua kikuu magerezani, na sera za kibaguzi dhidi ya wahamiaji walioathirika na TB.

Kauli mbiu mwaka huu ni "tuungane kutokomeza TB" lakini kuna baadhi ya nchi tatizo linazidi kuongezeka ikiwemo Tanzania kwa mujibu wa Dr Liberate Mleo meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini humo

Ameongeza kuwa makundi hatarishi ni kuanzia umri wa miaka 45 , maeneo ya vijijini, na vile vile kwa walioathirika na virusi vya ukimwi VVU, na anataja baadhi ya hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items