Na. Ahmad Mmow.
Wanachama wa chama cha CUF wilayani Lindi mjini, jana walipiga kambi kwenye ofisi yao ya wilaya ya nakuitaka kamati ya utendaji ya wilaya hiyo imtimue uanachama na imvue nyazifa zote za uongozi mwanchama mwenzao, Zainab Lipalapi anaetajwa kuwa aliteuliwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho anaetambuliwa na ofisi ya msajii wa vyama vya siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini ya chama hicho.
Wakizungumza na wajumbe wakamati ya utendaji ya wilaya hapo jana ndani ya ofisi ya wilaya hiyo iliyopo katika Manispaa ya Lindi. Walisema kitendo kilichofanywa na mwanachama mwenzao hakikubaliki. Kwa madai kwamba ni usaliti usiovumilika na unaositahili avuliwe nyazifa zote za uongozi alizonazo. Ikiwamo udiwani, uenyekiti wa wilaya hiyo wa jumuia ya wanawake na ujumbe wa kamati ya utendaji ya wilaya. Walisema Lipalapi hakusitahili kukubali uteuzi huo kwasababu anatambua kwamba wanachama na viongozi wa wilaya yake hawamtambui Profesa Lipumba kama mwanachama na mwenyekiti wa taifa. Kwasababu alishafukuzwa uanachama.
Mwanachama Hawa Kipara alisema Lipalapi hasithili kuendelea kuwa mwanachama na kushikilia nyazifa alizonazo. Hivyo kamati hiyo iketi haraka na kufanya maamuzi magumu kabla hajakivuruga. Hamisi Sapanga alisema msimamo wa viongozi na wanachama wilayani humo ni kutomtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa chama.
Kwasababu aliacha madaraka nafasi ya uenyekiti.Sapanga huku akinukuu vifungu kadhaa vya katiba ya chama hicho alivyodai vinadhihirisha Profesa Lipumba hakuwa na haki wala uwezo wakufanya uteuzi wa aina yeyote. Hivyo mwanachama huyo avuliwe uongozi na atimuliwe uanachama kama alivyofanywa profesa. "Tunamshanga mwanachama mwenzetu kusikia amekubali kuteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini na profesa Lipumba, ambae kwa makusudi ameamua kukivuruga chama chetu.
kwahiyo kamati ya utendaji iketi haraka na ichukue maamuzi magumu ya kumvua nyazifa zake zote na iliagize tawi lake limtimue uanachama hafai kuendelea kuwa kiongozi, "alisema Sapanga. Kauliza za wanachama hao ziliungwa mkono pia na madiwani wa kata za Mnazimmoja na Mingoyo ambao walidai kitendo kilichofanywa na diwani mwenzao nichafedheha na akivumiliki.
Mwenyekiti wa wilaya ambae aliwahi kuwa mbunge wa Lindi mjini, Salum Barwany licha ya kusema kamati ya utendaji itaitishwa haraka ili kujadili suala hilo na kulitolea uamuzi kwa mujibu wa katiba. Lakini pia alisema yeye na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya chama walifanya juhudi kubwa ya kumtafuta akiwa jijini Dar-es-Salaam ili atoe ufafanuzi na ingewezekana ilibidi akanushe kwa kutumia vyombo vya habari.
Hata hivyo juhudi hizo hazikuzaa matunda baada ya Lipalapi kuwapiga chenga. "Hatukupenda tufanye uamuzi wa pupa, ilibidi tusubiri arudi na tumuite na tumsikilize kwenye kikao cha kamati tendaji imsikilize na ifanye uamuzi kwa mujibu wa katiba yetu ya chama bila kumuonea, hiki ni chama haki sawa kwa wote.
Ushauri wa wanachama wenzetu tumeupokea, "alisema Barwany. Wakati viongozi na wanachama wakisema hivyo, Zainab Lipalapi anaetuhumiwa kuhudhuria baadhi ya vikao vilivyoitishwa na Profesa Lipumba nakukubali kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini. Alisema tuhuma anazotuhumiwa nazo nizauongo. Kwasababu hata yeye anasikia tu. "Nilikwenda hosipitali na nilitaka nikanushe mbele ya vyombo vya habari nikiwa Dar-es-Salaam, hata hivyo nilikosa muda, kama aliniteua hakunishirikisha na hakunijulisha.
Kwakweli amenifanyia vibaya namuomba aondoe jina langu kwenye orodha ya wajumbe wa bodi hiyo kama kweli aliniteua, alisema Lipalapi. Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vililiripoti kuwa Lipalapi aliteuliwa na Profesa Lipumba kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini ya CUF. Hali ambayo imesababisha hamaki na ghazabu kwa wanachama hao ambao chama chao hicho kilizoa viti vyote saba vya wenyeviti wa mitaa vilivyoshindaniwa ili kujaza nafasi wazi katika manispaa ya Lindi.