Boko Haramu yafanya shambulizi Cameroon

Watu watano na askari .mmoja wameripotiwa kufariki baada ya boko haramu kufanya shambulizi la kujitoa muhanga nchini Cameroon.

Kwa mujibu wa habari,shambulizi hilo limefanyika katika jimbo la Kolofata kaskazini mwa Cameroon.

Kiongozi wa eneo hilo Midjiyawa Bakari amesema kuwa magaidi hao wamesababisha kifo cha mwanamke mmoja na kuteka watoto watatu wa kike wakiwa na nia ya kukimbia nao Nigeria.

 Ripoti zinaonyesha kuwa Boko Haramu hupenda kufanya mashambulizi kama hayo katika nchi za jirani kama Niger,Cameroon,Benin na Chad.

Nigeria imekuwa ikishambuliwa na kundi la Boko Haramu toka mwaka 2009.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items