Kesi ya Mkurugenzi wa Jamii Forum yapigwa kalenda hadi Mei 2

Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo ya Kuzuia upelelezi iliyokuwa isikilizwe Jumatatu hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Mei 2, 2017.

UPANDE wa Mashtaka umewasomea maelezo ya awali Wakurugenzi waJamii Forumbaada ya kukamilisha upepelezi katika Kesi  inayowakabili ya kushindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi wa Jeshi la polisi.

Salumu Mohamedi wakili wa Serikali  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwasomea maelezo watuhumiwa hao.

Katika maelezo hayo wakili Salumu Mohamedi alisoma kuhusu umiliki wao wa mtandao wa Jamii forum, makazi yao , majukumu yao na kuhusu mashtaka yao.

Washtakiwa wote walikubali maelezo hayo.

hiyo namba 456 yenye shitka moja ambapo inadaiwa kuwa tarehe Mosi Aprili , tarehe 13 Desemba  mwaka huu, huko mikocheni wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaama akiwa kama  Mkurugenzi wa  Kampuni ya Jamii media inayoendesha mtandao wa jamii forum alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao huo  kwa Jeshi la polisi.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 2 mei mwaka huu
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items