Darassa
Mtayarishaji wa video nchini Hanscana ambaye pia ni mdau wa lebo ya CMG ya rapa Darassa amefunguka kuwa msanii huyo ameshindwa kuachia wimbo mpya mwezi huu kutokana na kuwa na show nyingi za kimataifa kumbana.
“Kusema kweli Darassa alikuwa aachie wimbo mpya mwezi huu lakini show za Rwanda na Burundi zimembana sana, amekuwa na tour ndefu sana katika nchi hizo na pia baadaye ataenda Kenya. Tour zikiisha tu ataachia kazi mpya kwa sababu ndani tuna kazi nyingi kali, ni kitendo cha kuzitoa tu,” alisema Hanscana
Rapa huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya kitendo ambacho kimewafanya mashabiki wa muziki kumsubiria kwa hamu.
