Kocha wa Chelsea asema Kipigo kimesisimua ubingwa

London, England .Kipigo cha mshitukizo cha Chelsea dhidi ya Crystal Palace kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kimefanya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England zizidi kuvutia, kwa mujibu wa kocha wa Blues. Antonio Conte.

Vinara hao wa Ligi Kuu walipigwa na mshangao kwa kipigo chao cha pili nyumbani msimu huu, wakati Palace ikifufua matumaini ya kutoshuka daraja kwa ushindi wa mabao 2-1.

Ushindi wa Tottenham dhidi ya Burnley ulimaanisha kuwa Spurs sasa inazidiwa pointi saba na Chelsea, ikiwa katika nafasi ya pili.

"Kwa vyombo vya habari, haya ni matokeo mazuri kwao, kwa sababu inafanya mbio za ubingwa kuvutia," alisema Conte.

"Lakini siku zote nimekuwa nikisema, ligi humalizika unapokuwa na hesabu nzuri za kuhakikisha kuwa umeshinda. Vinginevyo unatakiwa kupambana, unatakiwa kucheza kila mechi kwa kujaribu kushinda."
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Ujuwe Ugonjwa wa Busha

Kilimo cha Bamia