London, England.MASHABIKI wa Chelsea wamemchenjia mshambuliaji wao, Diego Costa na kumwambia kama vipi aende tu China baada ya kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika mechi ya Ligi Kuu England ya kipigo kutoka kwa Crystal Palace uwanjani Stamford Bridge juzi Jumamosi.
Chelsea ilitawala sehemu kubwa sana ya mchezo huo, lakini fowadi huyo Mhispaniola mwenye asili ya Mbrazili alipoteza nafasi za kufunga huku kikosi chake kikikubali kulala kwa kipigo cha mabao 2-1.
Wakati Chelsea ikichemsha na kushindwa kuendeleza pengo lake la pointi 10 dhidi ya timu inayofuatia, Tottenham imeshinda na kufanya pengo hilo kwa sasa kubaki pointi saba tu, jambo linaloanza kuwatia presha mashabiki wa timu hiyo kwenye mbio zao za ubingwa.
Straika Diego Costa hakuwa na siku nzuri na mashabiki hao wanamtaka Kocha Antonio Conte awe anampa nafasi pia Michy Batshuayi kabla ya kuamua kutumia kurasa zao za Twitter kumshambuliaji mshambuliaji huyo, ambaye ndiye kinara wa mabao kwenye kikosi chao katika ligi kwa msimu huu.
Mashabiki hao kila mtu aliandika anachojisikia kwenye Twitter kuhusu Costa, huku mwingine akidai kwamba umefika wakati tu wa fowadi huyo aende tu China kwa sababu anacheza uwanjani huku akili yake ikiwa kwenye mipango hiyo ya kuhamia China.
Mwingine alisema Costa ni mbinafsi na aliwanyima makusudi ushindi baada ya kushindwa kutoa asisti kwa Eden Hazard, ambaye alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga.