Mgogoro mkubwa wa wananchi wa kijiji cha Nyamichere kata ya Nyakunguru na mgodi wa dhahabu

Mgogoro mkubwa uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano kwa kuwahusisha wananchi wa kijiji cha Nyamichere kata ya Nyakunguru na mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya kamati ya tahthimin iliyoundwa na waziri wa nishati na madini Prof. SOSPETER MUHONGO kuazimia mgodi uwalipe wananchi 1,500 zaidi ya shilingi billion 11 kama fidia ya mazao yaliyofyekwa mgodi huo kwa lengo la kuanzisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo miaka mitano iliyopita.

Akitoa maazimio mbele ya wananchi wa kijiji hicho wakiwemo viongozi wa mgodi mkuu wa wilaya ya Tarime Bw. GLORIUOS LUOGA amesema kamati iliyoundwa na waziri wa nishati na madini Prof. SOSPER MUHONGO, imeutaka mgodi huo kuwalipa wananchi kiasi cha shilingi billion 11 kama sehemu ya fidia ya mazao badala ya shilingi billion 27 ilivyoelekezwa na kikosi kazi kilichowashirikisha wataalam wa ardhi wakiwemo baadhi ya wajumbe kutoka kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wakaonesha kufurahishwa na maazimio ya kamati hiyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items