F Mkude asema hasira zetu tutazishusha kwa Mbao | Muungwana BLOG

Mkude asema hasira zetu tutazishusha kwa Mbao

NAHODHA WA SIMBA, JONAS MKUDE.

NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude, amesema kuwa hasira za kupotez a mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar wanazitua kesho kutwa kwenye mchezo wao dhidi ya Mbao FC.

Simba itakuwa mgeni wa MbaoFC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ukiwa ni mchezo wa pili wa timu hiyo kanda ya Ziwa.

Akizungumza na gazeti hili jana muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazoezi ya timu hiyo, Mkude, alisema kuwa imewauma sana kupoteza mchezo wao na kagera Sugar uliowapelekea kutolewa kwenye kiti cha uongozi wa ligi na sasa wanataka kusahau hayo kwa kushinda mchezo wao wa Jumatatu.

"Bado kwenye nafsi zetu kuna kitu kinatuuma baada ya kupoteza mchezo wetu kule Bukoba.., ili kusahau yote tunapaswa kushinda kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Mbao.., tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo huu ili kurudisha furaha ya mashabiki wetu," alisema Mkude.

Aidha, alisema mbali na mchezo huo, pia wanataka kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu kwenye mchezo dhidi ya Toto African utakaochezwa siku nne baada ya mchezo huo wa Jumatatu.

"Lengo letu likuwa kuondoka hukuKanda ya Ziwa na pointi zote tisa, lakini kwa bahati mbaya tumepoteza pointi tatu..., tutahakikisha hizi sita zilizobakia tunaondoka nazo,"aliongeza kusema Mkude.

Aidha, alisema mashabiki wa timuhiyo kuwa na umoja na kuendelea kuiunga mkono timu yao kwa kuwa bado ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa.

"Pamoja na kufungwa na Kagera, bado tupokwenye mbio za ubingwa na tunaweza tukatimiza malengo yetu.., bado tuna michezo mingine mbele yetu na tumekuwa na utofauti mdogo wa pointi na timu inayoongoza ligi," alisema Mkude.

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 55 ikizidiwa kwa pointi moja na Yanga inayoongoza ligi.