Leo April 14 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekagua mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. ambapo amejiridhisha na kwamba siku ya kesho Wanadar es salaam waungane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika uzunduzi wa Hosteli hizo.
Kwa mujibu wa RC Makonda hosteli hizo ambazo zimegharimu shilingi bilioni 10 zitakuwa na uwezo wa kumudu zaidi ya wanafunzi 3,840, Ambapo kila mmoja atakuwa akilipa shilingi laki moja na elfu kumi tu kwa muhula mzima, ambapo aliongeza kuwa kiwango hicho ni cha chini ukulinganisha na kodi za hosteli zilizopo mitaani.
Katika hatua nyingine RC Makonda amearifu kuwa kesho mara baada ya Uzunduzi huo, Rais Magufuli pia ataweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa nyumba za Magomeni kota sambamba na uzinduzi wa mtambo wa kuandalia Zege.
PICHA ZA MUONEKANO WA HOSTELI HIZO NJE NA NDANI
PICHA: ALIPOTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA

![]() |
| Mtambo wa kuandalia Zege |






















