Tanesco kutowakatia umeme wadaiwa sugu walioonyesha nia

Dodoma. Shirika la umeme (Tanesco) Mkoani Dodoma, limesema kuwa halitawakatia huduma ya umeme wadaiwa  sugu ambao tayari wameahidi kulipa kidogo kidogo.

 Akizungumza na gazeti hili leo Ofisa habari wa Tanesco mkoa wa Dodoma, Innocent Lupenza alisema kuwa mkoa huo una wadaiwa sugu wengi lakini baada ya kufanya nao mazungumza wengine wameanza kulipa na kuahidi kumaliza madeni yao na hivyo kutowakatia huduma hiyo.

“Wapo wadaiwa sugu wengi zikiwemo Mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira lakini baada ya kufanya nao mazungumzo, wengi wameahidi kulipa madeni yao na wengine tayari wameshaanza kupunguza hivyo tumewapa muda wa kumaliza madeni yao na kama hawatafanya hivyo tutawakatia,” alisema Lupenza.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items