Viongozi wa matawi ya CUF wamtaka Lipumba ajiweke kando

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Profesa Ibrahim Lipumba ametakiwa kujiweka kando na shughuli za chama hicho kwa kuwa alishajiuzulu nafasi ya uenyekiti.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano) na baadhi ya viongozi wa matawi makubwa ya hamasa ya chama cha CUF, mkoa wa Dar es Salaam, wakati wakizungumza na wanahabari jijini hapa.

Miongoni mwa matawi hayo makubwa ambayo yapo zaidi ya 20 ni Chechnya, Osama Bin La den, Kosovo, Mwinyi Mkuu na  Saratoga

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa CUF, Tawi la  Mwinyi Mkuu Magomeni Rashid Abdullah  amesema  Profesa Lipumba siyo kiongozi wa chama hicho lakini amekuwa na tabia ya kuendesha vikao kinyume cha sheria ambavyo asilimia kubwa vinalenga kukihujumu chama hicho ili kishishinde uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019.
Mpya zaidi Nzee zaidi