Wananchi Lamadi kutumia Hati watakazopata kuombea mikopo benki

Serikali imeridhia wananchi wanaoishi katika mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu kuhakikisha wanapimiwa maeneo yao ili waweze kupatiwa hati miliki itakayosaidia kuongeza thamani ya makazi hayo na hivyo kuwawezesha kupatiwa mikopo inayotolewa na taasisi mbalimbali za kifedha.

Hayo yamesemwa na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Bw. WILIAM LUKUVI alipokua akizungumza katika ziara yake wakati wa kukabidhi hati kwa wananchi waliopimiwa makazi yao.

Lukuvi amesema uamuazi wa kutoa ofa hiyo imetokana na agizo alilopewa na rais JOHN POMBE MAGUFULI kama sehemu ya kusaidia wananchi kuishi katika makazi bora na hivyo kuongeza thamani ya makazi yao yakayowasaidia kupata dhamana ya mikopo katika taasisi za kifedha.

Kisha akatoa miezi miwili kwa watu elf tano ambao bado hawajapatiwa hati hizo kukamailisha taratibu zote ili na wao waweze kunufaika.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items