WAZIRI WA AFYA, UMMY MWALIMU.
WAKATI Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikisisitiza sula la watoto wenye umri chini ya miaka 5 kutibiwa bure katika hospitali nchini, hali hiyo ni tofauti katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.
Katika hospitali hiyo wazazi wa watoto waliolazwa hapo wanaambiwa wakanunue dawa za matibabukwenye maduka binafsi kwa ajili ya watoto wao kwa kuelezwa hakuna dawa za bure katika hospitali hiyo.
Hali hiyo imebainika baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo alipotembelea leo katika wodi ya watoto wenye umri kuanzia mwezi mmoja na kukuta wazazi wananunua dawa za kuwatibu watoto wao.
Tumbo alipewa malalamiko hayo na wazazi wa watoto hao alipotembelea hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa mashuka 50, sabuni za kufulia, mabeseni,biskuti na soda ambavyo vimetolewa na Taasisi ya Muheza Development Trust Found (MDTF) kupitia mbunge wa jimbo la Muheza Adadi Rajabu.
Mmoja wazazi hao Razia Hatibu alimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa tangu amefika katika hospitali hiyo kumuuguza mwanaye aitwaye Abduli
Jamali mwenye umri wa miezi saba amekuwa akiambiwa na madaktari akanunue dawa kwa ajili mtoto wake.
Katika kuthibitisha hayo, baadhi ya wazazi walimuonyesha Mkuu wa wilaya stakabadhi za malipo ambazo wamekuwa wakinunua dawa za watoto wao wadogo wa miezi miwili tangu walazwe hospitalini hapo.
Kufuatia malalamiko hayo, Mku wa Wilaya Tumbo aliagiza kupelekwa haraka dawa katika wodi ya watoto hao kwa kuwa watoto wadogo wanatibiwa bure.
Alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Muheza imeanzisha bohari ya dawa kwa mana hiyo ni lazima wahakikishe zinapatikana dawa za watoto ili
kuhakikisha hazikosekani katika wodi hiyo ya watoto wadogo katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake katibu wa hospitali hiyo, Neema Mudu alisema kuwa hospitali kwa sasa imezidiwa na wagonjwa wengi na mpaka sasa bado hawajapata mgao wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Madawa Tanzania (MSD) na ndio maana wodi ya watoto haina dawa.