Waziri Lukuvi afanya Uteuzi Wa Wajumbe Wa Bodi Ya Wakurugenzi Wa Shirika La Nyumba La Taifa (Nhc)

Kufuatia uteuzi wa Bibi Blandina S.J. Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25/02/2017. Mhe. William V. Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990, amewateua Wajumbe 7 wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa.

Aidha, uteuzi huu ni wa kipindi cha miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 23 Machi, 2017.

Majina ya wajumbe hao ni kama ifuatavyo:

Prof. John M. Lupala
Bwn. Gabriel Malata
Bi. Mary Mlay
Bi. Subira Mchumo
Bwn. Ally Hussein Laay
Bwn. Pius Maneno
Bwn. Kesogukwele Masudi Issa Miraji Msita


Imetolewa na:

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items