Waziri wa Lebanon matatani kufuatia kauli za chuki kuhusu Uturuki

.Waziri wa Utalii wa Lebanon Avadis Kadanian  ajipata mashakani baada ya kusema kuwa amefurahishwa na matatizo yanayokumba Uturuki kipindi hiki .

Waziri huyo ametakiwa kujiuzulu kufuatia kauli zake zilizotajwa kuwa za kibaguzi.

Siku ya Ijumaa waziri Kadanian alikuwa akizungumza katika kipindi cha mahojiano na televisheni ya MTV Lebanon ambapo alikiri kuwa yeye binafsi haipendi Uturuki na kwamba hawezi kuwakaribisha waturuki nchini Lebanon.

"Siwezi kuunga mkono kitu chochote kilicho na uhusiano na Uturuki ,iwe ni bidhaa zao au hata watu wao sina uwezo wa kuwazuia raia wa Uturuki kutokuja Lebanon lakini pia sina nia yakuwakaribisha katika uwanja wa ndege ."

Kadanian pia alisema kuwa atachagua Armenia alipoulizwa ikiwa akiwa katika hali ya kuwa afanye uchaguzi baina ya Armenia na Lebanon .

Kauli za chuki za waziri huyo zilizua hisia kali mitandaoni na kampeni ya kumtaka kujiuzulu ilianzishwa Twitter kwa alama ya reli '#Kadanianapologiseorresign'.

Ujumbe mmoja wa Twitter pia ulifahamisha kuwa 'Haiwezekani waziri wa Lebanon kuwa na kauli ya chuki kuhusu raia wa Uturuki wakati Lebanon na Uturuki zina uhusiano mzuri.'

Waziri wa zamani wa sheria Ashraf Rifi alimtaka Kadanian pia kujiuzulu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items