Kipigo cha bao 1-0 ambacho Azam imekipata kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho juzi, kimeinyima rasmi nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kwa ngazi za klabu mwakani, lakini huenda kikaondoka na vichwa kadhaa kwenye kikosi cha timu hiyo.
Baada ya kuteleza mapema kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ambayo bingwa wake huiwakilisha Tanzania Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho ndio nafasi pekee iliyokuwa imebakia kwa Azam kujitetea na endapo ingefika fainali, ingejiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Tathmini iliyofanywa na gazeti hili, washambuliaji watatu wa timu hiyo wako hatarini kupigwa panga.
Wachezaji hao ni Yahaya Mohammed, Samuel Afful na Khamis Mcha ‘Vialli’, wanategemea miujiza kubakia kwenye kikosi cha Azam msimu ujao kutokana na mchango duni walioutoa kwenye timu hiyo msimu huu.
Kocha msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche alikiri kuwa yapo mabadiliko ambayo yatafanyika kwenye kikosi chao ingawa hakutaka kuweka wazi nafasi hizo. “Hatuwezi kuwa kila mwaka tunashiriki na hakuna mafanikio,” alisema kocha huyo.