Uvccm Wamuunga mkono Rais Magufuli Kwa Hatua Alizochukua

Umoja wa  Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCMM), umenpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk .John Pombe Magufuli kwa kuonesha Uzalendo mkubwa alionao kwa nchi yake,baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi  katika sakata la zima la Makinikia.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu mkuu wa  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  alipokuwa akitoa salamu za pongezi za Vijana wote katika  ukumbi wa CCM vIJANA kinondoni .

Shaka amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa   uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi

“Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma,tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja    
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items