VIDEO: Rais Magufuli hana mamlaka ya kusamehe waliogushi vyeti- Wakili Jebra


April 27, 2017, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora) . Angela Kairuki alikabidhi rasmi Ripoti ya Uhakiki wa Vyeti ambapo iliripotiwa kuwa jumla ya watumishi 9932 wanatumia vyeti feki.
Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Rais Magufuli alitoa kauli kuwasamehe wale watakaojiondosha kazini wenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria na wale watakaoendelea kubaki kwenye nafasi zao.

Kauli hiyo imezua mijadala tofauti tofauti, ambapo Muungwana Blog imefanya mazungumzo na Wakili wa Kujitgemea Jebra Kambole ambapo kwa upande wake amesema "Kisheria Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu anayetuhumiwa kufanya kosa la jinai iwapo mtu huyo hajafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuhukumiwa,Madaraka pekee aliyonayo Mh. Rais ni kutoa Msamaha kwa wafungwa wanaotumikia kifungo (President's Prerogative of Mercy) kama alivyofanya hivi karibuni kwenye Sherehe za Muungano"

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI...



Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia