Wachimbaji wadogo wanne wafa na watatu wajeruhiwa Geita

Geita.Wachimbaji wadogo wanne wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya nyamalimbe yaliyopo wilayani Geita mkoani hapa.

Watu saba walifukiwa ambapo kati yao watatu wameokolewa na wamelazwa katika Kituo cha Afya Katoro.

Tukio hilo limetokea  saa mbili asubuhi. Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items