Wakazi wa Kinondoni Mahakamani wamelalakia maji yaliyozingira nyumba zao kutokana na baadhi ya wakazi hao kujenga katika mkondo wa maji.
Akizungumza leo mkazi wa eneo hilo Bi. Khadija Hamis amesema kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha wanapata adha kubwa ya maji hayo yanayotuama kwenye eneo hilo.
Amesema kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamezingirwa na maji kwa wiki mbili sasa na hakuna chochote kinachofanyika.
Aidha amesema kutokana na hali hii kuendelea ,wanaiomba serikali kutatua tatizo hili mara baada ya kuisha masika.




