Ardhi sasa kupimwa kwa kutumia picha za satelaiti

Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na  Taasisi ya misitu, (PFP)wamekuja na mpango wa kutumia picha za satelaiti kwa ajili ya upimaji na upangaji wa matumizi bora ya ardhi kwa ngazi ya vijiji.

Hayo yamesemwa leo (jumatano) na Kaimu Mkurugenzi wa tume hiyo Dk Stephen Nindi wakati wa uwasilishwaji wa taarifa iliyotekelezwa na PFP katika vijiji 19 vya mradi wa kutumia picha hizo.

Amesema mpango huo utapunguza migogoro ya ardhi ya muda mrefu na kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi kwa vijiji nchini.

Dk Nindi amesema ni hatua nzuri ya utekelezaji wa teknolojia hiyo na kwamba wananchi watafaidika nayo kwa kutambua mipaka yao halisi na kuona kiasi gani cha ardhi kimetumika na matumizi yake husika.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items