Gwiji Lothar Matthaus aitabilia Juventus ubingwa

London, England. Gwiji wa zamani wa Bayern Munich na Ujerumani, Lothar Matthaus ametabilia Juventus itaifunga Real Madrid na kutwaa ubingwa wa Ligi ya .

 Hii ni mechi ya fainali itakayovutia kuitazama na mashabiki yeyote mpenda soka.

Ni mechi itakayokutanisha klabu mbili bora duniani kwa sasa.

Naiona Juventus ikiwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa.

Tofauti ya timu hizi mbili Juve ni wepesi zaidi kubadilika kutokana na wakati kulinganisha na Real Madrid.

Real hakuna ubishi kwamba wanaweza kukupa majibu ya maswali magumu.

Lakini kama Juve itacheza katika kiwango kile ilichoonyesha wakati wa mechi za hatua ya mtoano, basi watakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

Walionyesha ubora wao dhidi ya Barcelona na Monaco wanaweza kubadili kutokana na mchezo pia mechi moja na nyingine.

Wanaukuta bora unaongozwa na Giorgio Chiellini, Leonardo Bonucci na Andrea Barzagli mbele ya kipa wao Gigi Buffon.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items