Marekani. Rais wa Marekani, Donald Trump, ameisifu nchi ya Saudi Arabia kwa kuitnga nchi ya Qatar inayotuhumiwa kuyasaidia kifedha makundi ya magaini.
Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza tishio la ugaidi.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Msemaji wa ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema mgogoro huo umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu.
"Kumekuwa na wasiwasi wa muda miongoni mwa nchi jirani na Qatar. Marekani inaendelea kuwasiliana kwa karibu na nchi zote ili kutatua mgogoro unaoendelea na kurudisha hali ya ushirikiano ambayo ni muhimu kwa usalama wa eneo.
“Nadhani, katika ujumbe wake, kuna hali ya kutilia mkazo suala la kudhamini ugaidi unaofanywa na baadhi ya nchi katika eneo hilo, lakini Marekani bado inataka huu mdororo wa uhusiano wa kidiplomasia utatuliwe haraka iwezekanavyo.” Amesema Spicer
Utiliti
*Qatar imetengwa na nchi zaidi ya sita za mataifa ya kiarabu
*Nchi hizo ni Yemen, Bahrain, Saudi Arabia, Libya na Umoja wa Falme za Kiarabu na Uturuki.
