WAKULIMA WA TUMBAKU WAPEWA USHAURI HUU





Na Omary Mngindo, Aliyekuwa Tabora

WAKULIMA wa zao la Tumbaku nchini wameshauliwa kuzingatia kuhifadhi zao hilo katika maghala yaliyoezekwa kwa nyasi ili kulinda ubora wake.

Rai hiyo imetolewa na Mtaalamu wa Tumbaku Alfred Lucas Mpulani akizungumza na Mwandishi wa habari hizi nyumbani kwa mkulima Mzee Adam Ndelele ikiwa ni ziara maalumu ya kujifunza namna ya kuandaa zao hilo linalotegemewa na wakazi wa Mkoa mzima wa Tabora.

Akiwa nyumbani kwa mkulima huyo, Mpulani alimwambia mwandishi kuwa zao hilo linapohifadhiwa kwenye nyumba iliyoezekwa kwa nyasi huwa na kwa kuanzia kinaiwezesha tumbaku kuwa katika ubora wa hali ya juu hiivyo kupata kilo za kutosha sanjali na pesa za uhakika.

"Hili zao la ajabu sana, halihitaji baridi wala joto kali, kwa mkulima anayelihifadhi kwenye nyumba iliyoezekwa kwa kutumia makuti anapata tumbaku yenye ubora na bei nzuri ukilinganisha na nyumba iliyoezekwa kwa bati," alisema Mzee Mpulani huku akiwataka wazingatie ushauri unaotolewa na wataalamu.

Nae Ridhiki Kabafu alisema kuwa wanajihusisha na kilimo cha zao hilo kwa miaka mingi laini kwa msimu huu jali si nzuri zana hali knayotokana na kutokuwepo kwa mvua ya kutosha, pia wakulima wengi walikata tamaa kutokana na hali hiyo.

"Nipo hapa kwa ajili ya kazihii ya kiliko, kwa mwaka nalipwash. Laki 4 malipo ambayo yanakidhi ukilonganisha  a kaziyenhewe, nawashauri vijana wenzangu tujikite katika shighuli zinazotupatia kipato halali badala ya kukaa vijiweni tu," alisema Kapafu.

Jafar Majala alisema kuwa baada ya shughuli za kilimo baada ya mavuno wanafunga kwenye mabalo na kuhifadhi katika maghala kabla ya kupeleka sokoni na kuwa bei nzuri inategemea  na kwamba ubora ukiwa mzuri bei inakiwa nzuri zaidi.

"Mvua ilikuwa chache hivyo tumbaku zilizokuwa hafifu zilikufa kutokana na jua kuwa kali kwa msimu huu, mwaka huu ukilinganisha na kilimo cha mwaka wa 2016 kwani mvua zilikuwa nyingi hivyo kustawi na kuwa na ubora zaidi.

Alimalizia kwa kutoa ushauri kwa wakulima kuwa msimu ujao wa kilimo ni vema wakaanza maandalizi mapema pia kuacha kukata miti na kuchoma moto kwa ajili ya maandalizi kwani hatua hiyo inasababisha kutonyesha mvua za uhakika.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items