Mbowe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa 'facebook' na kudai Prof Jay ni mpambanaji kwani amekuwa akiwapigania wananchi wa Mikumi pamoja na taifa kwa ujumla
"Katika harusi ya mbunge wa Mikumi, mbunge mjanja ni hakika wananchi wa Mikumi hawakufanya makosa kumchagua Mhe. Joseph Haule, kwani amekuwa mstari wa mbele kuipigania Mikumi na Taifa kwa ujumla wake. Harusi hii ilituunganisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali na vyama tofauti tofauti, hongera Mhe. Joseph Haule, kwa uamuzi uliofanya likiwa ni tukio kubwa katika maisha yako" alisema Freeman Mbowe
Profesa Jay alifunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililoko Posta jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo. Kisha baada ya hapo sherehe yao ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City huku ukihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu

