Zaidi ya kaya elfu kumi ziko hatarini kukosa makazi kutokana na nyumba zao za kuishi kujengwa katika eneo la shirika la reli TRL baada ya kuwekewa alama ya kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa na miundo mbinu mingine .
Baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora ambao nyumba zao zimewekewa alama ya kuvunjwa wakiwa katika nyuso za huzuni wameeleza masikitiko yao huku baadhi yao wakidai kuwa hawana mahali pa kwenda.
Mbali na kueleza masikitiko yao zaidi wanaelekeza kilio hiki kwa serikali wakihitaji msaada.
Wananchi hawa wamepewa notis na shirika la reli Tanzania kuhakikisha wanavunja nyumba hizo ndani ya siku thelathini kabla ya kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
Sakata hili la bomoa bomoa limeathiri maeneo mengi ya mkoa wa Tabora lakini kata zilizoathirika zaidi ni CHEYO, ISEVYA, KILOLENI , BACHU na MAPAMBANO zote zikiwa katika manispaa ya Tabora.