Na Omary Mngindo, Mkuranga
Halmashauri ya wilaya ya Mkranga Mkoa wa Pwani, Tanzania umekabidhiwa visima vinne virefu vyenye thamani ya zaidi ya sh. Mil 50 vilivyotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini.
Visima hivyo vinne vilivyokabidhiwa vimejengwa katika kijiji cha Kisayani, Kerekese, Mpafu na Sangasanga vilivyomo wilayani humo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Balozi wa Kuwait Jasem Al-Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait kupitia Ubalozi uliyopo nchini inafanya jitihada kubwa kusaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali zinazohusu Jamii ikiwemo afya pamoja na maji.
Aidha Balozi Jasem alisema katika kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli ya elimu bure wameamua kuanzisha mradi ujulilanao wa Kisima Kila Shule ili kupunguza changamoto ya maji pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama kwa wakati lengo, ni kuboresha elimu nchini.
"Maji ni muhimu sana, uchimbaji wa maji mashuleni sio utasaidia wanafunzi na wanachi wanaoishi karibu kunufaika na huduma hiyo, pia kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kupata huduma hiyo muhimu hivyo kuwapatia muda mzuri wa masomo", alisema.
Pia ubalozi huo umetoa mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya ya Mkuranga ili kuboresha huduma ya afya.
Aidha Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Vulu alisema afya ya Mama na mtoto ni muhimu sana hivyo kukikosekana vifaa afya ya mama itakuwa hatarishi.
"Tunashukuru sana kwa msaada wenu, huu utasaidia sana mama kujifungua mtoto mwenye afya pia na mama mwenyewe kubaki mwenye afya njema, tunawashukuru kwa ksaada huu* "alisema Vullu.
Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdalah Hamis Ulega amewashuru Wakuwait hao kwa msaada huo na kusema mpaka sasa wameshachimba visima ishirini na nne 25 visima vinane kati ya hivyo ni vya serikali, visima kumi na mbili na vya wahisani wa ARF na visima vinne ni vya Ubalozi wa Kuwait nchini na kimoja kutoka kwa wahisani wa nchini Saudia.
idha aliongeza kama Mbunge wa Mkuranga aliguswa na kuamua kutafuta wafadhili baada ya kupata barua kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kisayani juu ya uwezekano wa kufungwa kwa shule hiyo kutokana na changamoto ya maji, ndipo akawatafuta wafadhili hao ambao wamechimba visima virefu vinne vya maji wilayani humo," alisema.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filiberto Sanga alitoa wito kwa wanachi kuhakikisha wanakitunza kisima hicho kisiharibike.