Waziri ataka Maroli ya Mchanga Zanzibar Kupimwa



Waziri wa Kilimo,Maliasili,mifugo na uvuvi Zanzibar Hamad Rashid ameagiza kupimwa upya magari yote yanayofanya biashara ya mchanga kisiwani Pemba ili kutambua ujazo sahihi wa magari hayo kwa lengo la kuepusha udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Waziri Hamad ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwepo kwa magari makubwa na yenye uwezo wa kuchukua tani nyingi lakini zimekuwa zikiandikishwa kwa tani kidogo wakati alipo fanya ziara katika shimo la kuchukua mchanga Shumba Vyamboni katika mkoa Kaskazini Pemba ambapo amesema wasiwasi wake ni kuwa madereva hao wanapunguza tani za magari  yao kwa ajili ya udanganyifu na kukwepesha na kulipa mapato pungufu.

Mapema Afisa mipango idara ya misitu Pemba Mussa said bakari alitetea hoja hiyo na amemweleza waziri huyo kuwa licha ya wasiwasi walionao juu ya magari hayo vipimo vinaonyesha kuwa yako katika uzita sahihi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items