Ofisi ya Takwimu za Ajira Nchini Marekani, imesema, jumla ya ajira 209,000, zilizalishwa mwezi Julai mwaka huu, ambacho ni kiwango cha juu kuliko ilivyotarajiwa.
Aidha, kiwango cha ukosefu wa ajira kilishuka hadi 4.3% ikiwa sawa na mwezi Mei, ambacho ni kiwango cha chini kabisa tangu mwaka 2001.
Takwimu zinaonyesha kuwa, ajira katika sekta ya huduma za vyakula kama migahawa ilikuwa 53,000, ambapo inaelezwa sekta hiyo kwa mwaka huu imetoa ajira 313,000 huku ajira katika sekta za afya na biashara nazo zikishuhudia ongezeko kubwa la ajira.
Rais Donald Trump, ameeleza kufurahishwa na ripoti hiyo ambapo kupitia ukurasa wake wa twitter, ameandika kuwa idadi nzuri ya ajira Marekani na sasa ndio ameanza kazi.