Watu wanne wamefariki dunia na wengine 44 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbarali baada ya kuugua ugonjwa wa kipindupindu ambao umelipuka katika maeneo mbalimbali ya mji wa lujewa na vitongoji vyake wilayani Mbarali.
Mlipuko wa ugonjwa kipindupindu umetokea katika mji wa Lujewa wilayani Mbarali na kusababisha vifo vya watu wanne huku wengine 44 wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Mbarali kwa matibabu ya ugonjwa huo, ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi katika mji wa Lujewa wamedai kuwa mlipuko huo umesababishwa na muwekezaji wa shamba la mpunga la Mbarali Estate, kufunga mfereji mkuu wa maji ambayo yanategemewa na wakazi wa mji huo kwa matumizi ya majumbani hivyo kusababisha wananchi kuishi katika mazingira machafu.
Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune amesema amesema serikali inaendelea jitihada za kudhibiti ugonjwa huo na kwamba tayari changamoto ya uhaba wa maji kwenye mfereji wa muwekezaji imekwishatatuliwa baada ya kufanya mazungumzo na muwekezeji kumtaka afungulie maji ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amemuagiza mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya pamoja na timu yake ya afya kupiga kambi wilayani Mbarali ili kudhibiti ugonjwa huo, lakini pia akawataka wananchi kufuata maelekezo ya wataalam wa afya kwa lengo la kujikinga na kutokomeza kipindupindu wilayani Mbarali.