Waangalizi wa amani walio chini ya shirika la umouja wa Mataifa wamewasili nchini Sudan Kusini kwa lengo la kujaribu kuzungumza na viongozi wa taifa hilo ambalo limekuwa katika mgororo kwa muda mrefu.
Hata hivyo waangalizi hao wamesema kwamba kuna matumaini mazuri ya hali ya usalama kutokana na kupungua kwa mapigano na kuwataka viongozi kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa muda mrefu ambao umepelekea maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kukimbia makazi yao.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan kusini Kuola Manyang amesema kwamba licha ya kwamba kuna baadhi ya maeneo ya nchi hiyo bado mapigano yamekuwa yakiendelea lakini kama serikali imejipanga kuhakiksha kwamba wanarudisha amani chini ya serikali ya Rais Salva Kiir ambaye anaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.
Aidha kwa upande wake aliyekuwa makamu wa Rais wa Sudan kusini Bw. Riek Machar amesema kwamba mgogoro huo hauwezi kuisha kutokana na kwamba wasuluhishi wa mgogo huo wamekuwa wakipendelea upande wa serikali hali ambayo inazidi kuongeza chuki miongoni mwa jamii.