Wakati Operesheni maalum ya kukamata magari yenye Vioo vya Giza au Tinted iliyotangazwa na jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es sa;aam ikitarajiwa kuanza kesho baadhi ya wananchi wenye magari wameanza kutekeleza agizo hilo la kubandua karatasi za Giza katika vioo vya magari yao.
Chanel ten ilitembelea mitaa mbalimbali ya katikati ya jiji la Dsm ikiwemo barabara ya Lumumba ambayo ni maarufu kwa uuzaji na uwekaji Tinted kwenye magari na kushuhudia wimbi la vijana wakipata kazi mpya ya kubandua tinted hizo ili kutekeleza agizo la jeshi la polisi na kuepuka usumbufu.
Wakizungumza na Channel ten baadhi ya vijana waliokutwa wakitekeleza agizo hilo wamesema kwa upande mmoja wanaunga Mkono suala la kupmbana na uhalifu wanaotumia magari yenye Tinted huku upande wa pili wakionyesha kupoteza ajira za muda ambazo zimekuwa zikiwaingizia kipato.
Baadhi ya wamiliki wa maduka katika mtaa wa Lumumba wamedai kuingiza makontena yenye bidhaa hizo za Tinted na tayari wameshalipia ushuru na Kodi za serikali na kubaki njia panda juu ya zoezi hilo.