Paulinho akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la ushindi dakika ya 84 ikiwalaza wenyeji, Getafe 2-1 Uwanja wa Coliseum Alfonso Perez katika mchezo wa La Liga. Gaku Shibasaki alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 39 kabla ya Denis Suarez kuisawazishia Barca dakika ya 62.