Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua rasmi ujenzi wa ofisi za walimu 402 kwa mkoa wa huo, huku akiwataka wananchi na wadau wengine kuunga mkono jitihadRC a hizo.
Makonda ameyasema hayo leo alipotembelea katika eneo ambalo limetengwa maalumu kwa shughuli za ufyatuaji wa tofali Ukonga Magereza jijini humo.
"wenzetu waliwahi kupanga lakini hawakuweza kufanikisha suala hili la ujenzi ,lakini sisi hatutakubali kushindwa lazima tutafika mwisho tukiwa na matokeo mazuri"alisema Makonda.
Amesema watahakikisha ndani ya wiki hii inapatikana mifuko ya saruji zaidi ya elfu kumi sambamba na mafuta ya kuweza kusukumia mitambo ya kufyatulia matofali.
Nae Kanali Charles Mbuge ambae ni msimamizi mkuu wa kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu,ameelezea mafanikio waliyo yapata katika michango ya ujenzi huo ni milioni mia mbili ishirini na saba, laki tatu ,ishirini sita elfu na mia mbili.
Aidha ameelezea changamoto walizonazo ikiwamo ya kutoka katika baraza la mazingira NEMC kuhusu uchimbaji wa mchanga katika mto mpiji, upungufu wa mafuta wa mara kwa mara ,upungufu wa malori unaosababisha kushindwa kufanya kazi nyakati za usiku ambapo kazi hizo hufanywa usiku na mchana ,upungufu wa vibao vya kufyatulia tofali ,ambapo idadi inayohitajika ni vibao elfu kumi, sambamba na ukosefu wa magari ya utawala.
"Mkuu wa Mkoa ametoa wazo la kusimamia maendeleo hayo kwa sababu anawependa watanzania wote hasa wana Dar es salaam"Alisema Kanali Charles.
Aidha amewasa wadau na wapenda maendeleo kuendelea kusaidia ili kutatua changamoto hizo na kufanikisha mradi huo wenye tija kubwa kwa Taifa.



