Serikali ya Uingereza yasitisha ushirikiano wake na Myanmar

Serikali ya Uingereza yasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar

Serikali ya Uingereza imefahamisha kusimamisha  ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.

Serikali ya Uingereza ilikuwa ilikuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshÅŸ la Myanmar.

Waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May ametangaza kuwa serikali yake inasitisha ushirikiano huo wa kijeshi na Myanmar.

Hayo waziri mkuu wa Uingereza aliyafahamisha katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York.

Theresa May amesema kuwa Uingereza inasikitishwa na vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Myanmar ammapo waislamu wa jamii ya Rohingya ni waathirika.

Aliendelea kusema kuwa Bi Aung San Suu Kyi anatakiwa kutamka wazi kuwa operesheni zinazoendeshwa zisitishwe haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya waislamu 421 000 kutoka jamii ya Rohingya wamekimbilia nchini Bangladesh  tangu kuzuka kwa mauaji Agosti 25.
Mpya zaidi Nzee zaidi