Vijana watakiwa kukitumia kikamilifu chuo cha mafunzo ya usafiri wa anga

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA,bwana Hamza Johari katika mahafali ya kumaliza mafunzo ya kozi namba 37 ya ‘Taarifa za Usafiri wa Anga’ ambapo wahitimu 17 wamemaliza.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu hao bwana Hamza Johari amewaasa wahitimu hao,ambao wengi wao wanatoka nchini Uganda, kutumia mafunzo waliyopata kuboresha zaidi sekta ya usafiri wa anga nchini mwao na Afrika Mashariki.

Chuo cha Kimataifa cha mafunzo ya usafiri wa anga, ambachO kinatambuliwa na NACTE na mabaraza mengine yanayosimamia taaluma za usafiri wa anga duniani, kinachukua wanafunzi kutoka Uganda, Botswana, Swaziland, Rwanda, Lesotho na nchinyingine za Afrika.
Mpya zaidi Nzee zaidi