Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa bodi ya Arsenal itaangalia upya wajibu wake kama meneja wa klabu hiyo.
Raia huyo wa Ufaransa alisaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuiongoza Arsenl kwa miaka 21.
Lakini akiongea leo Alhamisi kwenye mkutano mkuu wa kila mwaka wa klabu hiyo alisema kuwa mazungumzo yatafanyika wakati mkataba wake utaisha.
"Ninataka kuona kile bodi inafikiria kuhusu matokeo yangu," Wenger alisema.
"Baada ya hilo tutaamua penye tutaelekea. Matakwa yangua kawaida yamekuwa ni kuheshimu mikataba yangu."
Msimu uliopita, Arsenal walimaliza katika nafasi ya tano katika ligi ya Primia, na kushindwa kufuzu kwa Champions League.
Hiyo ndiyo mara kwanza Arsenal walishindwa kumaliza katika nafasi nne za kwanza tangu Wenger ajiunge na Arsenal mwaka 1996.
Wakati wa kumalizika kwa msimu Wenger alikabiliwa na shinikizo za kumtaka aondoke baada ya Arsenal kumaza pointi 18 nchini ya mabingwa Chelsea.