Mambo yazidi kuwa magumu kwa Bale

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amethibitisha kuwa nyota wa timu hiyo Gareth Bale ataendelea kuwa nje ya uwanja kwa muda huku akishindwa kuweka wazi endapo nyota huyo atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa wiki ijayo dhidi ya Tottenham.

“Pamoja na leo kuanza mazoezi mepesi lakini bado siwezi kusema atarejea uwanjani hivi karibuni kwasababu anahitaji mapumziko zaidi ili aweze kurudi akiwa kamili kiushindani”, amesema Zidane.

Bale aliumia majuma kadhaa yaliyopita kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund ambapo pia alikosa mechi ya mwisho ya taifa lake ya Wales ya kuwania kufuzu kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Kwa upande mwingine mchezaji mwingine wa Real Madrid mlinzi wa kulia Dan Carvajal amepona na ameanza mazoezi huku kocha Zidane akithibitisha kuwa ataanza kuonekana kwenye mchezo dhidi ya Tottenham wiki ijayo.

“Mchezaji ambaye tunajivunia amerejea ni Dan Carvajal, amepona matatizo yake ya maambuzi ya virusi ambavyo vilikuwa vimezunguka Moyo wake na kuathiri utendaji kazi bora wa Moyo lakini amepona na sasa yupo tayari kuanza kucheza”, ameeleza Zidane.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items