Dar es Salaam. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetenga jumla ya Sh75 milioni kusaidia huduma bora za maji safi, afya na elimu kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 30 na TPA, imemkariri Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Deusdedit Kakoko akisema fedha hizo ni sehemu ya majukumu ya mamlaka kusaidia inayowazunguka.
Amesema hayo mara baada ya kuzindua moja ya visima vitatu vilivyotolewa na mamlaka hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini.
“Tuna jumla ya bandari 90 nchi nzima na hizo zote inabidi zinufaike kutokana na misaada hii, na ndio maana unaona tunatoa kidogo kidogo kama tulivyofanya leo hapa,” amesema.
Amesema kwa Ziwa Victoria pekee kuna jumla ya bandari 30 wakati Ziwa Tanganyika kuna bandari 25 na Ziwa Nyasa bandari 15.
Amesema bandari zilizobaki ziko kwenye ukanda wa Bahari ya Hindi
“Kwa kanda ya ziwa peke yake tumetoa mashuka ya wagonjwa kwenye hospitali za mikoa, vituo vya afya na zahanati, na kwa upande wa elimu tumetoa madawati kwenye shule za msingi mbalimbali pamoja na kujenga visima vya maji safi,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, vijijini, Mwantumu Dau ameishukuru TPA kwa msaada huo kwani umechangia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Amesema hali ya upatikanaji wa maji katika Halmashauri hiyo imeongezeka kutoka asilimia 62.4 kwa Julai, 2016 hadi kufikia asilimia 65.4 kwa mwezi Oktoba, 2017.
“Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa miradi mipya ya maji iliyokamilika katika vijiji 10 pamoja na mradi huu wa visima vitatu tunaokabidhiwa leo,” amesema.
Amesema ili kutunza vyanzo vya maji, wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wananchi jinsi ya kutunza vyanzo hivyo pamoja na kutoa elimu ya utunzani wa mzingira.