Na Omary Mngindo, Lugoba
MADIWANI katika Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameelezea kukerwa kwao kutokana na kusuasua kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo wakati fedha zinatengwa lakini hazipelekwi kwenye miradi husika.
Madiwani hao wameelezea kukerwa huko katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 2017/2018 ambapo walisema pamoja na halmashauri yao kuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato lakini fedha wanazoziidhinisha ziende katika utekelezaji wa miradi hazifiki hivyo miradi mingi kusuasua.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ametumia muda mwingi kuchangia mada hiyo ambapo alielezea kusikitishwa kwake kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi licha ya madiwani hao kuidhinisha fedha ziende katika miradi lakini hazifiki.
"Hapa katika Makabrasha ukiangalia inaeleza kuwa miradi iliyotekelezwa ni sawa na asilimia 11 tu kwa maana yake yote ambayo tumeyaadhimia katika vikao vyetu hayajatekelezwa, hivyo hii yote itakuwa viporo," alisema Ridhiwani.
Kufuatia hali hiyo, Ridhiwani amewataka wataalamu na watendaji idara mbalimbali kuacha tabia hiyo badala yake kuhakikisha wanaelekeza nguvu zao katika kuikamilisha miradi yote ambayo inasuasua kabla ya kumalizika kwa mwaka wake wa fedha ili isiingiliane na bajeti ijayo.
"Halmashauri yetu inakusanya zaidi ya sh. Mil 300 kwa mwezi, kwa miezi mitatu sh. Mil.900 nashangazwa na kitendo cha kutopelekwa fedha ambazo sisi madiwani kupitia vikao vyetu tumeidhinisha lakini hazifiki, hapa kila mradi inaonesha fedha hazijafika wakati tayari tumeaazimia zipelekwe kukamilisha miradi husika," alisema Ridhiwani.
Juma Mpwimbwi Diwani wa Kata ya Miono alihoji inakuwaje Halmashauri inakusanya mapato ya kutosha lakini hazifiki katika miradi husika huku akitaka nguvu zaidi zielekezwe katika utekelezaji wa miradi hiyo iweze kukamilika mapema kwani ukusanyaji hauendani na utekekezaji wa miradi husika.
Nae Rehema Mwene Diwani wa Kata ya Lugoba amesikitishwa kwa kitendo cha kutofikishwa kwa fedha kiasi cha sh. Mil. 400 zilizotakiwa kupelekwa katika zahanati ya Lugoba lakini mpaka sasa hazijafika huku akishindwa kufahamu kipi kinachosababisha hivyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Zikatimu alisema kiasi cha sh.milioni 225 zilitengwa kwa ajili ya miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na tayari baadhi ya miradi inaendelea kutekelezwa.