Rais Trump:Sitawahi kumuita Kim Jong Un mfupi na mnene

Rais wa Marekani Donald Trump ameandika katika mtandao wake wa twitter kuwa hatawahi  hata siku moja kumuita rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mfupi na mnene.

Kwa mujibu wa habari rais Trump amelalamika na kuandika kuwa Kim Jong Un amemuita mzee.

Trump amezungumza hayo baada ya kuhudhuria mkutano wa APEC Vietnam.

Marekani na Korea  Kaskazini zimekuwa katika mzozo baada ya Kim Jong Un kufanya mara kwa mara majaribio ya makombora ya nyuklia.

Rais Trump amekuwa akimuonya Kim Jong Un mara kwa mara bila mafanikio yoyote.

Aidha Pyongyang imeahidi kuendelea na utengenezaji wa makombora licha ya kuwa imewekewa vizuizi na Umoja wa Mataifa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items