Wakulima hatarini kuugua kipundupindu


WAKULIMA wengi wanaozalisha mpunga na mbogamboga kwenye skimu ya Mtambo iliyoko Hai mkoani Kilimanjaro hawana vyoo.

Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Watumiamaji na Utunzaji Mazingira (Uwamasakwa) Frank Kimaro, amewaonya kuwa ikiwa hawatajenga vyoo vya kisasa na kuvitumia upo uwezekano wa kupata magonjwa ya mlipuko.

Alizungumza hayo na wananchi wa vijiji vya Chekimaji, Kawaya na Mkarama vilivyopo wilayani Hai, wakati wa ziara ya kutembelea mfereji wa kilimo cha umwagiliaji skimu ya Matambo.

Aidha, alikuta changamoto nyingi ikiwamo hiyo ya ukosefu wa vyoo katika maeneo hayo ya kilimo cha umwagiliaji.

Kimaro alisema wakati umefika kwa wakulima hao kuanza kujenga vyoo vya kisasa bila kubweteka kwa kusubiria fedha kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi huo.

“Wakulima wa mpunga hamna budi kutumia sehemu ya fedha mnazopata kwenye mpunga kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu ambayo yanaweza kutokea kutokana na maji na mazingira kuchafuliwa na kinyesi,”alionya na kuendelea:

“Baadhi ya wakulima wa mpunga wa maeneo haya hawana vyoo wengi wao wanajisaidia kwenye maji wanapokuwa katika mashamba hayo hivyo kujiweka kwenye hatari ya kusababisha magonjwa ya mlipuko,”alisema Kimaro.

Mfereji wa Mtambo una jumla ya matawi 11 ya umwagiliaji ambayo itatumika kumwagilia ekeri 300 na zaidi ya wakulima 5,000 wa vijiji vitatu wananufaika na kilimo hicho cha umwagiliaji cha mpunga na mboga mboga.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkalama,Joseph Mzomo alisema kuwa mwaka juzi serikali iliwataka wakulima hao kuuchimba vyoo lakini
hadi leo hawajachimba na kuonya kuwa wanaweza kusababisha janga.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items