Klabu ya Simba leo inashuka katika dimba la uwanja wa Taifa saa 10:00 jioni kusaka pointi 3 dhidi ya klabu Majimaji kutoka mkoani Ruvuma katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguuko wa 15.
Kocha mkuu wa Klabu hiyo, Pierre Lechantre amepanga kikosi kwa kuanza na nahodha John Bocco , Kapombe, Juuko na Mwambeleko huku Mzamiru na Mavugo wakipigwa benchi.
Kwa sasa wekundu hao wa msimbazi wanaongoza ligi kwa alama 32 wakiwa mbele ya klabu ya Azam FC wenye alama 30 wakiwa wapo mbele kwa mchezo mmoja.

